UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS)

VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS)_*


Nini maana ya vidonda vya tumbo?
Ni vidonda vilivyo wazi ambavyo hutokea katika kuta za tumbo,sehemu ya juu ya utumbo mdogo au kwenye kuta za koromeo kutokana na bacteria waitwao H.pylori na asidi inayozalishwa kwenye kuta za tumbo.
Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito. nk


CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
⤵⤵⤵⤵⤵⤵
Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ila vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;

Ø Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
Ø Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin(bayer), (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
Ø Msongo mawazo (stress)
Ø Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
Ø Kunywa pombe na vinywaji vikali kupitiliza.
Ø Uvutaji wa sigara.
Ø Kuto kula mlo kwa mpangilio maalumu
Ø Kansa ya tumbo

KUNA AINA TATU YA VIDONDA VYA TUMBO.

1⃣ VIDONDA NDANI YA TUMBO.(GASTRIC ULCERS)
Hivi ni vidonda ambavyo hutokea ndani ya tumbo,kwenye kuta za tumbo.

2️⃣ VIDONDA NDANI YA KOO (ESOPHAGEAL ULCERS)
Hivi ni vidonda ambavyo hutokea ndani ya koo la chakula,kwenye kuta za koo la chakula.

3️⃣ VIDONDA KATIKA UTUMBO MDOGO (DUODENAL ULCERS)
Ni vidonda ambavyo katika sehemu ya juu ya utumbo mdogo uitwao duodenum
📎 NI KWA NAMNA GANI BACTERIA (H.pyori) Husababisha vidonda vya TUMBO

⤵⤵⤵⤵⤵⤵⤵

-Bacteria, Helicobacter pylori/Campilobacter pylori anaweza kusafiri kutoka kwa mtu Mmoja kwenda kwa mwingine kupitia njia zifuatazo:
⤵⤵⤵

(a).📎Kupitia mate (kunyonyana midomo)
(b).📎Kupitia matapishi.
(c).📎 Kupitia kinyesi
(d).📎Kupitia chakula ama maji yaliyokuwa na bacteria hawa.

SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA MTU KUAMBUKIZWA BACTERIA HAWA (H.pylori)

⚫ Kuishi mazingira yenye mikusanyiko mkubwa wa watu bila kuchukua tahadhar.
⚫ Kunywa maji yasiyokuwa safi.
⚫ Kula vyakula visivyooshwa mfano matunda na Mboga za majani.
⚫ Kuishi karibu na mtu mwenye vidonda vya tumbo bila kuchukua tahadhar.

H.pylori anapoingia katika mwili wa binadamu huathiri uzio mwenye kulinda ukuta wa tumbo na utumbo mdogo (protective mucous) hali hii hupelekea kudhoofika kwa kuta katika tumbo na utumbo mdogo. Ukuta huu unapodhoofika husababisha Tindikali (Asidi) inayozalishwa tumbo kuunguza na kuuchimba ukuta wa tumbo pia Bacteria hawa huchimba ukuta wa tumbo na KUSABABISHA kutokea vidonda katika ukuta wa tumbo na vidonda hivi ndivyo tunavyoviita vidonda vya TUMBO kwasababu vipo tumboni (Gastric Ulcers)

⚫ Bacteria huyu haathiriwi na Acid ya tumboni ( Hydrochloric acid~HCL) kwasababu ana uwezo wa kuzalisha kimeng`enya (Urease enzyeme) ambayo huungana na UREA kuzalisha Ammonia ambayo huungana na Acid ya tumboni (HCL) kuzalisha Maji na Ammonium Chloride ambayo haina uwezo wa kumuathiri huyu Bacteria. Hivyo bacteria huyu huzidi kujilinda kwa namna hii Mpaka hufikia hatua ukuta wa tumbo huchimbwa zaid na huyu Bacteria huzid kuingia ndan zaid ya tumbo ambapo acid hushindwa kumuathiri na hali hii husababisha vidonda vya TUMBO kuzid na KUSABABISHA mgonjwa kuwa na hali mbaya zaid.

⚫ Huyu Bacteria huathiri zaid kwa pamoja na Acid ya tumbo na hufikia hatua mgonjwa huweza kupata Kansa ya tumbo/Kansa ya Utumbo mdogo.


.📎 NI KWA NAMNA GANI MATUMIZI YA MARA KWA MARA YA DAWA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU KAMA Aspirin(Bayer),(NSAIDs),(Advil,Aleve nk) HUWEZA KUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO?

⤵⤵⤵⤵⤵⤵⤵⤵

-Katika mwili kimeng’enya kiitwacho Cyclooxygenase( COX) ambacho hupatikana sehemu mbalimbali kama vile kwenye mishipa ya damu,misuli nk.COX Hufanyakazi ya kuzalisha hormone iitwayo Prostaglandins ambazo kazi yake kubwa ni kuzalisha uteute ambao hufunika kuta za tumbo na utumbo mdogo kwaajili ya kukinga kutokana na madhara ya Acid ya tumbo na bacteria mbalmbali .

Haya Madawa ya kutuliza maumivu yanapotumika mara kwa mara hupelekea kuzuia uzalishaji wa kimeng’enya Cyclooxygenase (COX) hivyo hali hii husababisha kutozalishwa kwa Prostaglandins na kupelekea kupatikana udhaifu katika ukuta wa tumbo na matokeo yake husababisha urahisi wa tumbo kushambuliwa na Bacteria pamoja na Acid ya tumboni (HCL).

Hivyo kutumia mara kwa mara madawa ya kutuliza maumivu si salama kwa afya yako.


KWANINI MAZIWA/CREAM SIO RAFIKI KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO*??

Jawabu
⤵⤵⤵⤵⤵⤵
⚫ Maziwa yana kiasi kingi cha madini ya Calcium (Ca),madini haya huchochea uzalishwaji wa acid kwa wingi tumboni,hali hii hupelekea vidonda kuchimbika zaidi na baadae husababisha hali kuwa mbaya zaid kwa mgonjwa.

⚫ Wengi wakitumia maziwa hupata naafuu ya muda kwasababu ya ile hali ya maziwa kuvifunika vidonda kwa muda na baada ya hapo hali huwa mbaya.Hivyo maziwa si salama kabsa kwa wagonjwa wa vidonda vya TUMBO.

⚫ Hapo zamani madaktari walikuwa wakishauri maziwa kwa mgonjwa wa vidonda vya TUMBO lakin tafiti zinaonesha kwamba maziwa si salama kabsa kwa mwenye vidonda vya tumbo, ukiona daktari anakupa USHAURI huu basi huenda akawa hajui ama hajafikiwa na tafiti za wakati huu.
VYAKULA AMBAVYO SI RAFIKI KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

⚫Pombe
⚫Kahawa
⚫Maziwa/Cream
⚫ Nyama yenye mafuta mengi
⚫ Vyakula vilivyokaangwa(kwa mafuta mengi)
⚫ Vyakula vyenye viungo vingi
⚫ Vyakula vyenye chumvi nyingi
⚫ Vyakula vyenye acid kama vile Malimao,ndimu nk
⚫ Nyanya pamoja na bidhaa zake.
⚫ Chocolate
⚫ Vyakula vikavu
⚫ Vyakula vyenye gesi nyingi kama maharage,maziwa nk.


KWANINI BAADHI YA WATU WAKINYWA MAZIWA HUHARISHA??

Jawabu
⤵⤵⤵⤵⤵

⚫ Kuna baadhi ya watu miili yao haina uwezo wa kukamilisha mmeng’enyo wa Sukari aina ya Lactose katika maziwa na bidhaa za maziwa.Hali hii huitwa Lactose intolerance. Kushindwa kukamilisha mmeng’enyo wa Lactose hupelekea mwenye hali hii Kuharisha,tumbo,tumbo kuuma,kichefuchefu,tumbo kujaa gesi na Kivimbiwa baada ya kula ama kunywa bidhaa zinazotokana na Maziwa (Diary products). Hali hii pia huitwa lactose malabsorption.

Lactose intolerance ina aina nne,ambazo ni⤵
1.📎Primary Intolerance
2.📎Secondary intolerance
3.📎Developmental intolerance
4.📎Congenital intolerance

⚫ Hivyo, hali hii haina maana kwamba mwenye vidonda vya tumbo ndio hupata bali INAWEZA kumtokea yeyote ambae mwili wake una uwezo mdogo wa kukamilisha mmeng’enyo wa Sukari (Lactose) inayopatikana kwenye maziwa na bidhaa.
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO

⚫Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na kuendelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vina dalili kama:⤵⤵⤵

1.📎 Kupata maumivu ya tumbo ya kuwaka moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
2.📎 Kupatwa na kiungulia(heartburn) karibu na chembe ya moyo
3.📎 Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
4📎 Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
5.📎 Kupata haja kubwa ya rangi ya kahawia au nyeusi cheenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
6.📎 Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
7.📎 Kushindwa kupumua vizuri.
8.📎Kuharisha hasa unapokula vyakula vinavyochochea vidonda vya TUMBO.
9.📎Kupata choo kigumu kama cha mbuzi
10.📎 Maumivu ya mgongo
11.📎 Tumbo kuwaka moto.
12.📎 Kupungukiwa damu na kupelekea kupata kizunguzungu.
13.📎 Mwili kudhoofika na kupungukiwa kilo
14.📎 Dhakari(Uume) kulegea/kusinyaa na kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
15.📎Mapigo ya moyo kwenda mbio.
16.📎 Macho kupunguza nguvu ya kuona vizuri.


UFANYEJE ILI KUTATUA TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO.


Ili mtu atumie dawa ya vidonda vya TUMBO na kupona anatakiwa kuzingatia yafuatayo:⤵⤵

1.📎 Apate dawa sahihi (yenye uwezo wa kutibu vidonda vya TUMBO)

2.📎 Ajiepushe na vichochezi vya Vidonda vya TUMBO.vichochezi hivyo ni kama vile⤵
-Msongo wa mawazo (Stress)
-Vyakula visivyokuwa rafiki kwa mwenye vidonda vya tumbo basi. Hapo utakuwa umemaliza shida ama kulipunguza kwa kiasi kikubwa.

Dr. LIWAYA
Tiba Asili Tanzania.
Simu.0755162724.

Published by Pandex Herbal Natural

"Tunawasaidia wahanga wa magonjwa mbali mbali kwa kuwaelimisha juu ya magonjwa yao,matibabu kwa kutumia mimea tiba,vyakula na Ushauri"

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started